TUNAUZA SURA EH?!

 

photos  
TUNAUZA SURA EH?!
Meneja wa bendi ya muziki wa dansi ya T-Respect, Ali Choki (wapili kutoka kulia) akiwa katika harakati za kurekodi picha za Video ya wimbo wake “Mfano kwa vijana” pamoja na wanenguaji maarufu kutoka bendi mbalimbali akiwemo Aisha Madina (Kulia) kutoka Afican Stars Twanga Pepeta.Hii ilikuwa ni jana ndani ya viunga vya Hotel ya kisasa ya Atriums Sinza Africa Sana Jijini Dar es Salaam.

FULL KUJIACHIA NDANI YA ATRIUMS HOTEL
TUNAUZA SURA EH?!
Baadhi ya wanenguaji waliokuwa wakimpa tafu Ali Choki wakati wa zoezi hilo la uchukuaji wa picha za Video wakiwa wamejiachia katika bustani za kuvutia zilizopo katika viunga vya Hotel ya Utriums .

AISHA MADINDA KUMBE BWANA MISOSI
TUNAUZA SURA EH?!
Pamoja na unene alionao, Aisha Madinda bado anakandamiza misosi kwa kwenda mbele. Kamera yetu ilimnasa jana akikandamiza chips nyama choma alizoagiza nje ya hoteli hiyo kukwepa gharama. Aliyenaye ni mtoto wa kaka’ke.

AJALI
TUNAUZA SURA EH?!
Basi hili la abiria linalofanya safari yake kati ya Mbagala na Mwenge Jijini Dar es Salaam lenye namba za usajili T 708 ACJ lilinaswa na kamera yetu jana jioni likiwa limepata ajali mbaya maeneo ya Mtoni kwa Azizi Ally Temeke, wakati dereva wa basi hilo alipokuwa akijaribu kuikwepa pikipiki aina ya Bajaji.Watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Temeke.

MWANAUME KUIMBA
TUNAUZA SURA EH?!
Kiongozi wa kundi la muziki wa mipasho la New Zanzibar Stars Modern Taarab, Ahmed Mgeni akivamia jukwaa wakati wa onesho kabambe la kundi hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Ikweta Mtoni Temeke Jijini Dar es Salaam.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s


%d bloggers like this: