Mtangazaji mahiri wa michezo wa TBC Baruani Muhuza akitangaza live mechi ya Stars na Ivory Coast. Maulidi Baraka wa Kitenge wa ITV na Radio One yuko pembeni akifuatilia mchezo
Katibu Mkuu wa Tff Fredrick Mwakalebela wakiwa na furaha na watanzania walioko Abidjan kuishangili stars baada ya gemu usiku huu
mashabiki wakishangilia taifa stars mara tu baada ya kipyenga cha mwisho kulia dakika chache zilizopita huko abidjan katika wanja la felix houphet boigny. kwa niaba ya wadau wote globu ya jamii inatoa shukrani za dhati kwa mdau huyu anayetuletea vitu laivu toka huko. mdau ubarikiwe kwani umeweza kutuweka karibu na huko mliko!
NA MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAA!!!!!!!
TAIFA STARS INATOKA KIFUA MBELE KWA KUIDUNGUA IVORY COAST BAO 1-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUENDELEA MBELE KATIKA MICHUANO HII YA CHAN.
STARS INAONDOKA NA POINTI 3 NA JUMAMOSI ITAPAMBANA NA ZAMBIA MJINI BWAKELI KATIKA KIPUTE KINGINE AMBACHO IKISHINDA ITAKUWA NA POINTI 6 NA IKITOKA SARE ITAKUWA NA POINTI NNE NA KUENDELEA KUWA KIONGOZI WA KUNDI HILI KWANI ZAMBIA WALITOKA TASA YA 0-0 NA WANA POINTI 4 (SAMAHANI SIO MOJA KAMA NILIVYOBOFYA AWALI). NDIO KUSEMA LAZIMA TUWAPIGE ZAMBIA (SIO SARE) KUWA NA UHAKIKA WA KUSONGA MBELE.
WADAU SAMAHANI HIYO LINK YA AWALI ILONESHA GEMU KWA MUDA KISHA IKAKATA.
ILA KULIKUWA NA HII
NIMEIPATA MAPEMA ILA SEMA MTANDAO ULIPATA KWIKWI MARA TU BAADA YA HAFTAIMU. ILA SI VIBAYA UKIITUNZA LINKI HIYO KWA AJILI YA GEMU ZIJAZO KWANI LIBENEKE NDIYO KWANZAAAAAA LINAANZA….
SAMAHANI SANA WADAU
MATOKEO YOTE NA RATIBA ZOTE

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s


%d bloggers like this: